Polisi wa kutuliza hali wametumwa eneo la Natooli mjini Naivasha baada ya mapigano kuzuka na kusababisha kifo cha mtu mmoja, wengine kadhaa kujeruhiwa na zaidi ya mbuzi 400 kuibwa. Inadaiwa mapigano hayo yalizuka baada ya jamii mbili kuzinazozozania kipande kimoja cha maelfu ya ardhi. Katika kisa hicho nyumba kadhaa zimeteketezwa moto. Wenyeji wanataka hatua za haraka kuchukuliwa kukabili hali. Mwili wa mwendazake ungali katika eneo la tukio
The post Polisi kutumwa Natooli kudhibiti usalama appeared first on Mediamax Network Limited.